Pamoja na kuangushwa, Amir Khan ameonyesha yeye ni
mpambanaji hasa baada ya kuinuka na baadaye kumshinda kwa pointi Julio Diaz.
Katika pambano hilo lililochezwa usiku wa kuamkia
leo, Khan mwenye miaka 26 amefanikiwa kumtwanga Diaz ambaye alimuangusha katika
raundi ya nne na kupoteza matumaini ya mashabiki wa Mwingereza huyo.
Baada ya Khan kuangushwa, mashabiki wake walijua
mambo yangeendelea kuwa mabaya kama ilivyokuwa katika mapambano mawili
yaliyopita dhidi ya Lamont Peterson na Danny Garcia ambayo yote alipoteza.
Baada ya kuinuka, Khan ambaye hiyo ni mechi yake ya
pili chini ya kocha mpya, alionyesha kubadilika na kupigana kwa kushambulia
zaidi huku ngumi zake nyingi zikimpata Diaz.
Wakati wa matokeo yanatangazwa, bado mashabiki wa
Khan walionekana hawana uhakika kama alikuwa ameshinda kwa hofu ya kuangushwa
katika raundi ya nne.











0 COMMENTS:
Post a Comment