Hakuna ubishi tena kwamba ushindi wa leo wa Yanga wa
mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro umeivua Simba ubingwa wa Tanzania Bara.
Simba iliyojaa migogoro, ina pointi 35 na michezo
mitano ukiwemo wa kesho dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Iwapo Simba itashinda mechi zake zote tano, ina
uwezo wa kufikisha pointi 50 wakati tayari Yanga imefikisha 52.
Maana yake, Simba inaweza kugombea nafasi ya pili
iwapo haitapoteza mechi ya kesho. Kama itafungwa na Azam pia itakuwa ni wiki
ngumu kwake kwa kuwa itakuwa imeondolewa tena kuwania nafasi ya pili.
Azam ikishinda itafikisha pointi 49, wakati Simba
itakayokuwa imebakiza michezo minne, ikishinda yote itakuwa na 47.
Simba chini ya Ismail Aden Rage imeandamwa na
migogoro ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi kujiuzulu.
Hivi karibuni ilimtimua kocha wake, Milovan Cirkovic
ambaye amerejea kwa Serbia na kumpa nafasi Mfaransa, Patrick Liewig ambaye
kikosi chake kimekuwa kikisua.
Pia Simba imeingia mgogoro na wachezaji wake wengi
wakongwe ingawa tayari Felix Sunzu na Mwinyi Kazimoto waliokuwa wamondolewa
kikosi kama ilivyo kwa akina Haruna Moshi, Ramadhani Chombo, wamerudishwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment