Full time:
MPIRA UMEKWISHAAAAAAA
Dk 90*2, kipa Ally Mustapha wa Yanga anafanya kazi
ya ziada kuokoa shuti la Majaliwa Sadick, inakuwa kona lakini ambayo haikuzaa
matunda.
Dk 89, Bahanuzi anainua mpira juu, pamoja na kumpita
kipa lakini unakwenda pembeni ya lango. Juhudi za Kiiza kuuwahi zinashindwa
kuzaa matunda.
Dk 83 Yanga wanafanya shambulizi ambalo halikuzaa
matunda baada ya krosi nzuri ya Nizar kutua kwa Kiiza lakini hakuwa makini
Dk 79, Yanga inamtoa Msuva anaingia Nizar Khalfan
Dk 59-63 Yanga inatumia muda mwingi kwa kupiga pasi
za shoo huku mashabiki wake wakishangilia kwa nguvu.
Dk 57, Yanga inalazimika kufanya mabadiliko kwa
kumtoa Bahanuzi baada ya kugongana na kipa wa Oljoro, anaingia Said Bahanuzi.
Dk 50, Oljoro wanamtoa kipa Mussa Lucheke, anaingia
Shaibu Issa
HALF TIME YANGA 3-OLJORO 0
GOOOOO dk 43, Yanga wanaachiana pasi maridadi na
mwisho Kiiza anakimbia na mpira na kumchambua kipa wa Oljoro kuandika bao la
tatu.
Dk 32, Yanga inamtoa Juma Abdul aliyeumizwa na Idd Saleh na nafasi yake ya beki wa kulia inachukuliwa na mkongwe, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa akishangiliwa sana na mashabiki wa Yanga wakati akipasha misuri.
Dk 24, Kavumbagu anashindwa kufunga baada ya kupokea
pasi nzuri ya Msuva akiwa katika nafasi nzuri ya kuipatia Yanga bao la tatu.
Dk 24, Kavumbagu anashindwa kufunga baada ya kupokea
pasi nzuri ya Msuva akiwa katika nafasi nzuri ya kuipatia Yanga bao la tatu.
GOOOOO Dk 19, viungo wa Oljoro wanapoteza mpira na
Msuva anauchukua, anawakimbiza mabeki wanne wa Oljoro na kuandika bao la pili
kwa shuti kali.
Dk 15, Oljoro wanajaribu kupeleka shambulizi langoni
mwa Yanga, hata hivyo wanaonekana kuwa dhaifu na wasio na madhara.
Dk 14, Shambulizi kali katika lango la Oljoro, krosi
murua ya Kiiza inamkuta Msuva lakini shuti lake linapaa sentimeta chache juu ya
goli.
Dk 7, Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi
mfululizo huku mabeki na viungo wa Oljoro wakiwa wamerudi nyuma.
GOOOOO dk 5 anafunga kwa kichwa baada ya kona
iliyochongwa na Niyonzima.
Dk 3, Yanga wanaanza na shambulizi kali langoni mwa
Oljoro, shuti kali la Msuva linapanguliwa na kipa na kuwa kona.
Vikosi vimerudi vyumbani, tayari kwa ajili ya kuanza
mechi.
Big Up Salehe kwa live show yako...umetusaidia sana wa ughaibuni tuliokua na hamu ya kufuatilia mtanange wa uamuzi wa nani atakua bingwa
ReplyDelete