April 28, 2013




Waliokuwa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi kwa kuwachapa Polisi Moro kwa mabao 2-1.

Polisi walitangulia kupata bao katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kupitia Admini Bantu katika dakika ya 10.

Lakini Simba walibadilika na kuanza kushambulia mfululizo hadi walipopata bao la kusawazisha katika dakika ya 34 kupitia kwa Haruna Chanongo ambaye alipokea pasi ya Amri Kiemba aliyeng’ara katika mchezo huo.

Mrisho Ngassa aliyekuwa anaisumbua ngome ya Polisi alifunga bao la pili la Simba katika dakika ya 48 baada ya kuiwahi pasi nzuri ya beki wa kulia Said Nassor ‘Chollo’.
Kila upande uliendelea kukosa nafasi lakini mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu ndiye alionekana kichekesho kutokana na kupoteza nafasi nyingi za wazi.

Wakati mwingine, mashabiki wa Simba walilazimika kumzomea Sunzu kutokana na kupoteza nafasi nyingi za wazi ikiwemo ile aliyobaki na kipa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic