Azam
FC imeng’oka katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kukubali kipigo
cha mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wake AS FAR.
John
Bocco ndiye aliyefunga bao pekee la Azam FC, lakini ndiye akaiangusha baada ya
kukosa mkwaju wa penalty katika dakika ya 81.
Iwapo
Azam FC ingepata mkwaju huo wa penalty aliopiga Bocco, basi ingekuwa imesonga
mbele kwa nafasi ya bao la ugenini kwa kuwa katika mechi ya kwanza, matokeo
yalikuwa sare ya bila kufungana.
Waamuzi
kutoka Algeria, aliyekuwa kati Abib Charef Medh aliyesaidiana kazi na na
Mahmoud Bitam na Mohamed Mekous mwanzo alionekana kama kuibania Azam FC ‘kiana’.
Lakini
baadaye alijirekebisha na kuacha kipigwe kwa uhakika na Azam FC wanapaswa
kujilaumu wenyewe kwa kukubali kutolewa.
Baada
ya Bocco kuifungia Azam FC, mashabiki wa Rabat walifanya vurugu lakini
wakathibitiwa na askari polisi uwanjani hapo na dakika chache baadaye wakapata
bao la kusawazisha kupitia Abdelrahim Achchakir aliyefunga kwa mkwaju wa penalty.
Abib
Charef Medh akamlika kadi nyekundu Achchakir katika dakika ya 35 baada ya
kumchezea ‘undundu’ Mganda, Brian Umony.
Azam
walipata pigo baada ya David Mwantika kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 57
na baada ya hapo, wenyeji wakazisidha mashambulizi makali.
Beki
mwingine wa Azam FC, Waziri Salum naye akamuangusha Kaddioiu Yuossef katika
dakika ya 74 na kulimwa kadi nyekundu.
Azam
FC walibaki wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa iliyo
chini ya Caf, maana yake Bongo inabaki mikono mitupu.
Kikosi
Azam FC:
Mwadini
Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Bolou,
Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba na
Brian Umony/Khamis Mcha ‘Vialli’.
AS FAR Rabat:
Ali
Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui
Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salahedine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui,
El Kodry Yassine, El Bakali Medamine na El Yousfi Mostafa.
0 COMMENTS:
Post a Comment