Barcelona ni noumaa, amini usiamini! Siku mbili baada ya kumsajili Neymar
wa Brazil, tayari jamaa wameishaanza kuuza jezi zake.
Kuonyesha timu za Ulaya zinajua biashara, jezi za Neymar, mgongoni zikiwa
na namba 11 zimeshaingia sokoni na zinanunuliwa kwa kasi kubwa.
Awali jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Thiago Alcantara lakini sasa
amekabidhiwa Mbrazil huyo ambaye usajili wake ndiyo gumzo zaidi kwa La Liga,
msimu huu.
Barcelona tayari ‘imefunga naye ndoa’ kwa miaka mitano na anatarajiwa
hivi karibuni kutua na kuanza kazi na klabu yake hiyo mpya.
Mashabiki wa Barcelona walionekana kuwa na furaha kumpata mshambuliaji
huyo wa Santos ambaye ndiye maarufu zaidi nchini Brazil kwa kipindi hiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment