May 28, 2013




Taarifa zilizozotufia sasa hivi zinaeleza msanii maarufu wa muziki wa hip hop, Albert Mangwea amefariki dunia.

Taarifa hizo zinaeleza Mangwea amefariki dunia katika hbospitali ya St Hellen iliyo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

“Tumepata hizo taarifa kwamba Mangwea amefia hapo St Hellen, lakini bado hatujajua tatizo ni nini hadi sasa.

“Lakini tunaendelea kufuatilia ili kupata uhakika zaidi. Lakini rafiki yake wa karkibu anayeishi hapa amesema ana uhakika kwamba Mangwea alilazwa hapo na amefariki dunia leo hii,” alisema Joshua ambaye ni mdau wa blog hii.

Bado tunaendelea kufuatilia kujua kuhusiana na hali halisi ya tukio hilo linalomhusu msanii huyo aliyeanza kutamba na songi la Ghetho Langu kabla ya kupoteza kabisa na Mikasi.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic