Kocha Mkuu
wa Yanga, Ernie Brandts ametua jijini Barcelona kwa lengo la kula bata tu,
akiwa ameongozana na mkewe.
Brandts
raia wa Uholanzi ameiambia Salehjembe kwamba ameamua kwenda Barcelona kwa ajili
ya kubadili mazingira.
Lakini
pamoja na hivyo, ametaka kula bata akiongozana na mkewe ili awe kamili
atakaporejea nchini kuanza maandalizi.
“Nitakaa
hapa kwa siku kadhaa kabla ya kurejea Uholanzi, niliona hapa ni sehemu nzuri ya
kubadili mazingira.
“Narudi Dar
mwanzoni mwa mwezi ujao, lakini hapa nimebakiza siku tatu kabla ya kurudi
nyumbani,” alisema Brandts.
Msimu huu,
Brandts ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea APR ya Rwanda, amefanikiwa kuipa
ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Pamoja na
hivyo ameiwezesha kulipa kisasi kwa kuifunga Simba mabao 2-0 katika mechi ya
kufunga msimu.
Hata hivyo,
mashabiki wa Simba wamekuwa wakikubali kufungwa na watani wao lakini
wakisisitiza bado hawajalipa ukubwa wa kipigo cha mabao 5-0 walichokipata Yanga
katika mechi ya mwisho kufunga msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment