Pamoja na kuwekwa benchi, kipa mkongwe wa Real Madrid, Iker Casillas amesema hataondoka.
"Maisha yangu ya baadaye yako hapa Real Madrid, nimeishi hapa tokea nikiwa na miaka tisa, hapa ni nyumbani, ndiyo sehemu nataka niwepo,” alisema Casillas na kuongeza.
“Kila kitu tulichopata, tunajivunia. Kama bunafsi na timu, pia klabu kwa ujumla. Nguvu tunaelekeza kuhakikisha tunatwaa taji la Copa del Rey. Itakuwa kazi ngumu lakini tunataka kushinda kwa ajili ya mashabiki wetu ambao wamekuwa wakitusapoti kwa kila hali.”
Hivi karibuni Casillas alikuwa katika mgogoro mkubwa na Kocha Jose Mourinho, hali iliyosabisha aendelee kumuweka benchi.
Kitendo cha kuwekwa benchi Casillas kimekuwa kikiwashangaza wengi na Mreno huyo ameamua kumtumia Diego Lopez.
Kutokana na hali hiyo kukawa na taarifa kwamba huenda Casillas akaondoka Madrid na kujiunga na timu nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment