Mashabiki wa klabu ya PSG ya Ufaransa, wameamua kuwahi hata kabla ya uongozi wao haujazungumza na Kocha Carlo Ancelotti kwa kumuandikia barua.
Mashabiki hao ambao wameona kama uongozi wao unachelewa, wameandika barua hiyo wakimtaka Ancelotti abaki na kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Barua hiyo ya wazi iliyotupiwa katika mtandao wa kijamii wa PSG, imeeleza kuwa mashabiki wana hofu, ndiyo maana wameamua kuandika barua hiyo.
Sehemu ya barua hiyo inasema hivi: “Tuna hofu huenda ukaondoka, imewahi kutokea kwa makocha wengine bora kama Kombouaré. Ndiyo maana tumefikia kuandika barua hii kwako kwamba tunafurahishwa na kazi yako hata katika Ligi ya Mabingwa tulikuwa kati ya timu bora zenye kiwango cha juu.
“Kazi yako nzuri inaonekana na tunaithamini sana, tunajua ulitaka kuanza na kutengeneza safu imara ya ulinzi na umefanikiwa lakini tunaamini msimu ujao utakuwa na kikosi bora kuliko chenye uwezo mkubwa zaidi katika ushambuliaji.”
Bado Ancelotti hajajibu kuhusiana na barua hiyo lakini mashabiki hao wana matumaini makubwa kwamba atarukdi.
0 COMMENTS:
Post a Comment