May 3, 2013




Chelsea wamefanikiwa kufuzu katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya kuwazamisha Basel ya Uswiss kwa mara ya pili.


Chelsea wamefanikiwa kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda kwa mabao 3-1 katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Europa League kwenye Uwanja wa Stamford Brigde jijini London. Wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-2.


Kutokana na ushindi huo, Chelsea sasa inakutana na Benfica ya Ureno ambayo imefuzu kwa kuichapa Fenerbahce ya Uturuki kwa mabao 3-1. Katika mechi ya kwanza, Waturuki hao wakiwa nyumbani walishinda bao 1-0. Hivyo Benfica wamefuzu kwa jumla ya mabao 3-2.

Fainali ya michuano hiyo itapigwa Mei 15 kwenye dimba la Amsterdam Arena jijini Amsterdam nchini Uholanzi.  


Katika mechi ya kwanza mjini Basel, Chelsea wakiwa ugenini waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Wakati katika mechi hiyo ya leo, Chelsea walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 baada ya Salah kuifungia Basel bao katika dakika ya 45.

Chelsea ikarejea katika kipindi cha pili na kasi ya kimondo na kupata mabao yake kupitia kwa Torres katika dakika ya 50 na Moses dakika ya 52.


Wakati Basel bado wanajiuliza kutokana na kufungwa mabao hayo ya haraka, beki Luiz alifunga bao la tatu katika dakika ya 59 baada kupewa pasi nzuri na Lampard na kupiga shuti lililoingia kwenye kona ya goli huku kipa akiangalia kama ‘kideo’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic