Borussia Dortmund na Bayern Munich zimekutana katika mechi
yao ya Ligi ya Ujerumani, Bundesliga na kutoka sare ya bao 1-1 lakini vituko
vingi vikatawala.
Mechi hiyo imechezwa jana Jumamosi, kivutio zaidi ilikuwa ni
namna makocha wa timu hizo walivyobadili vikosi vyao ikiwa ni pamoja na kupanga
wachezaji wengi wageni.
Hali hiyo inatokana na kwamba, timu hizo ndiyo zilizoingia
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley
jijini London, England.
Dortmund iliyokuwa nyumbani ilichezesha wachezaji sita tu wa
kikosi cha kwanza wakati wageni Bayern wakachezesha wacheza watatu tu wa kikosi
cha kwanza.
Dortmund maarufu kama BVB waliwapumzisha Sven Bender, Mats
Hummels, Lukasz Piszczek na Marco Reus. Ilkay Gündagon akatolewa katika dakika
ya 13 tu wakati wageni wao Bayern waliwapumzisha Arjen Robben,
Bastian
Schweinsteiger, Dante, Philipp Lahm,
Javi Martinez,
Thomas Müller, Mario
Mandzukic na Franck Ribery.
Wakati mechi inaendelea taarifa zikaeleza kiungo mkongwe Schweinsteiger
na Robben waliungana na Rais wa klabu yao, Uli Hoeneß mjini Munich kuangalia
mechi ya mpira wa kikapu kati ya Bayern Munich dhidi ya ALBA Berlin.
Katika mechi hiyo BVB walipata bao lao
mapema tu baada ya Nuri Sahin kupiga pasi ndefu kwa Jakub Blaszczykowski
aliyepiga krosi nzuri iliyomkuta Kevin Großkreutz aliyefunga bao matata na
kumuacha kipa Manuel Neuer
akiwa amezubaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment