Floyd Mayweather amerudi ulingoni na kufanikiwa kushinda
pambano lake la kwanza akitokea jela. Ameshinda kwa pointi 117-111, 117-111 na 117-111.
Mayweather amemshinda Roberto Guerrero kwa pointi
katika pambano la raundi 12 ambalo alilitawala kwa karibu raundi zote tokea
mwanzo katika pambano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa MGM Grand jijini Las
Vegas.
Pambano hilo lilikuwa ni la kuwania mkanda wa WBC
katika welterweight na sasa welterweight
amefikisha mapambano 45 bila ya kufikisha.
Mayweather alikuwa akimpiga Guerrero ngumi za
kushtukiza hali iliyomfanya wakati mwingine achanganyikiwe.
Kazi ya Mayweatherilikuwa ni kupiga ngumi na kutoka
haraka, wakati Guerrero alipoteza ngumi nyingi sana kutokana na umahiri wa
mpinzani wake wa kukwepa.
Mayweather amerejea ulingoni mara ya kwanza ikiwa
miezi 12 tokea apigane pambano lake la mwisho pia ni mara yake ya kwanza
kuzichapa ulingoni baada ya kuwa ametoka jela alikokumbana na kifungo cha miezi
miwili.
0 COMMENTS:
Post a Comment