May 5, 2013




Mlezi wa Simba, Rahm Al Kharusi leo anakutana na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short kwa ajili ya mkutano unaweza kuzaa neema kwa klabu hiyo.

Short na Rahma maarufu kama Malkia wa nyuki watafanya mkutano wao leo mjini Newcastle nchini England.

Malkia wa nyuki atasafiri kwenda Newcastler akitokea London alikotua juzi, tayari kwa mkutano huo.


Rafiki wa karibu wa Malkia wa nyuki amesema mwanamama huyo ngangari ambaye amepewa mwaliko huo na Short tayari amejipanga vilivyo na mkutano huo.

“Kila kitu kinakwenda vizuri na Malkia anausubiri kwa hamu, lengo lake kubwa ni kuhusiana na suala la maendeleo ya Simba.

“Kuna mambo mengi watajadili kuhusiana na maendeleo ya Simba, lakini uhusiano wa kudumu wa klabu hizo mbili.

“Kwanza sasa Malkia ametoka kidogo, ningeweza kukupa uzungumze naye ili kujua nini kinaendelea zaidi,” alisema mtu wake huyo wa karibu.

Katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam kati ya Short na Malkia wa nyuki, mmiliki huyo wa Sunderland alionyesha kuvutiwa na mwanamama huyo hasa katika masuala ya mipango ya maendeleo ya timu.

Short alichukua uamuzi wa kufanya mazungumzo zaidi na Malkia wa nyuki kuhusiana na suala hilo.

Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeiunganisha Simba na mmiliki huyo wa Sunderland ambaye alitua nchini akiwa mgeni wake.

Lakini akaamua kuwaunganisha na Simba na mara ya kwanza alizungumza na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kabla ya kufanya mazungumzo mara ya pili na Malkia wa Nyuki na mwisho akaamua kutoa mwaliko huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic