Ligi Kuu Bara inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa
mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24
kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya
mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina
pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.
Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa
katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye
pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.
African Lyon yenye pointi 19 katika
nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo
inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni
nyekundu.
Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza
kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba.
0 COMMENTS:
Post a Comment