Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakilalama kwamba Kocha
Mkuu wa Simba, Patrick Liewig ana shati moja tu la rangi nyeupe.
Mbaya zaidi wamekuwa wakisonga mbali zaidi kwa kudai
shati la kocha huyo halijapimwa saizi na halimtoshi.
Mfano wao ni kwamba akichomekea linatokelezea vibaya,
hivyo huenda anapaswa kushauriwa.
Salehjembe ilimhoji mara moja, jibu la Liewig liliwa
hili: “Sijaja kuzungumzia shati au mavazi, kama hauvutiwi na nilichovaa shauri
yako, mimi sijali.”
Lakini katika mechi kati ya Simba dhidi ya Polisi
Moro, ‘mtu mzima’ Liewig alitoka kivingine na kuwafunga midogo mashabiki wa Yanga.
Safari hii alipiga ‘pensi’ safi nyeupe akiachia mguu
kidogo, halafu akapiga raba kali ya chata kubwa ya Nike.
Raba hiyo ilikuwa ‘ikimechisha’ kitu cha Nike na ‘pulova’
la raungi nyeusi na ndani ilionekana alikuwa ana kitu kingine cheupe ingawa
ilikuwa si lahisi kukijua.
Salehjembe linaamini nguo iliyokuwa ndani ya ‘pulova’
haikuwa ile shati yake, itakuwa ni nguo nyingine mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment