Liverpool imefanikiwa kumnasa mshambuliaji hatari wa Celta Vigo ya Hispania, Iago Aspas kwa mkwanja wa pauni milioni 7.7.
Aspas atacheza mechi yake ya mwisho ya La Liga akiwa na Celta dhidi ya Espanyol, Jumamosi na baada ya hapo atakwea pipa kwenda England kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na Liverpool.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, msimu huu ameifungia Celta Vigo mabao 12 katika La Liga lakini alikuwa msumbufu kwa mabeki waliokutana naye.
Ukali wake ulizifanya timu kama Swansea na Valencia zitoe ‘jicho’ lakini mwisho Kocha Brendan Rodgers akafanikiwa kushinda vita hiyo na kufikia makubaliano na klabu pamoja na mshambuliaji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment