Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta atawaongoza wenzake leo wa kikosi cha TP Mazembe kupambana kulipa deni la mabao 3-1 waliyofungwa na Orlando Pirates jijini Johannesburg, Afrika Kusini wiki chache zilizopita.
Tayari Orlando Pirates wameishatua mjini Lubumbashi na wamejiandaa kuondoka mjini humo saa mbili tu baada ya mechi yao itakayopigwa kuanzia saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
Mazembe wanalazimika kushinda mabao 2-0 ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa na kutimiza ndoto yao ya kuwa mabingwa wa Afrika tena.
Lakini wana kazi kubwa ya kuizuia Orlando yenye washambuliajia viwembe kama Collins Mbesuma raia wa Zambia ambaye alifunga mabao mawili katika mechi ya kwanza mjini Johannesburg.
Waamuzi kutoka Shelisheli ndiyo wamepewa kibarua hicho cha Mazembe na Orlando, atakayekuwa kati ni Bernard Camille (mwamuzi wa kimataifa kuanzia mwaka 2011), wasaidizi wake ni Gilbert Lista na Hensley Danny ambao ni waamuzi wa kimataifa tokea 2010 na 2009. Mwamuzi wa akiba atakuwa ni Nelson Emile aliyepata nafasi ya kazi ya kimataifa kuanzia mwaka jana.
Mechi nyingine zikazochezwa leo Jumapili ni hizi zifuatazo na matokeo ya mechi za kwanza yalivyokuwa.
St George – Zamalek (1-1)
Al Ahly – CA Bizerte (0-0)
0 COMMENTS:
Post a Comment