May 24, 2013




Hakuna tena ubishi kwamba safari ya kocha Patrickl Liewig imefikia kikomo.

Tayari Mfaransa huyo yuko kwao na uongozi wa Simba umemkabidhi mikoba Abdallah Kibadeni.

Kibadeni aliyekuwa anainoa Kagera Sugar, huenda akaanza kazi ya kuinoa Simba ndani ya wiki mbili zijazo.

“Kweli kwa sasa kocha ni Kibadeni, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo,” kilieleza chanzo.

Lakini Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga naye alithibitisha kwamba uongozi wa timu hiyo ulifanya mazungumzo na Kibadeni ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuimarisha benchi la ufundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic