May 6, 2013



Malkia akiwa na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short katikati pamoja na mmoja wa walimu wa timu za vijana wa klabu hiyo

  *Watembelea viwanja vya watoto, wafanya mkutano na mmiliki

Viongozi wa Simba, leo wameshuhudia timu ya vijana ya Sunderland chini ya miaka 18 ikiiangamiza Newcastle katika mechi iliyochezwa leo mjini Newcastle.
 
Sunderland wakihenyeshana na Newcastle mbele ya Rage na Malkia wa nyuki..

Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa mazoezi na vijana wa Sunderland na mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi na mwenyekiti, Ismail Aden Rage walishuhudia mechi hiyo.


Ragena Malkia walikuwa wageni waalikwa wa mmiliki wa Sunderland, Ellis Short.


Wakiwa pamoja na mmiliki huyo, Rage na Malkia wa nyuki walishudia mechi hiyo iliyochezwa asubuhi kabla ya kupata nafasi ya kutembelea vifaa mbalimbali vya michezo vya klabu hiyo.

Wakiongozana na Short, waliongozwa na mmoja wa walimu wa timu za watoto kuangalia viwanja na vifaa vingine ambavyo hutumika kwa mafunzo.

Tayari Malkia na Rage wamekutana na Short na kujadili masuala kadhaa ya kuanzisha uhusiano wa klabu hizo mbili.

Baada ya hapo walipata nafasi ya kupumzika na leo usiku watakuwa kati ya wageni watakaohudhuria mechi ya Ligi Kuu England kati ya Sunderland dhidi ya Stoke City.
 
Malkia na Short

Sunderland chini ya Muitaliano, Roberto Di Canio itakuwa na kibarua kigumu cha kujikwamua kuteremka daraja kwa kutaka kupata ushindi.

Di Canio alianza vizuri lakini mambo yaliharibika baada ya timu yake kupokea kipigo cha mabao 6-1 katika mechi iliyopita.
 
Fatma 'Nyuki mtoto'

Hata hivyo, Muitaliano huyo amesema vijana wake watapambana leo na kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.




Short alitoa ndege yake ya kifahari kuwabeba Rage, Malkia wa nyuki pamoja na binti yake aitwaye Fatma maarufu kama Nyuki mtoto.

Baada ya kutua Newcastle wakitokea London, walipata fursa ya kuzungumza na milionea huyo kwa mara nyingine kabla ya kwenda uwanjani hapo na kushuhudia mechi hiyo, pia kuangalia vifaa vya klabu hiyo hasa kwa upande wa vijana.




Huenda wakazungumza tena na kiongozi huyo kesho mara baada ya mechi ya leo usiku ambayo inampa presha kwa kuwa anataka kuona timu yake inabaki Ligi Kuu England.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic