May 6, 2013



 Msanii maarufu wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz, usiku wa kuamkia leo alishuhudia Barcelona ikijiweka katika nafasi nzuri ya kubeba ubingwa wa Hispania kwa kutoa kipigo cha mabao 4-2 kwa Real Betis.


Mechi hiyo ya Ligi Kuu Hispania, maarufu kama La Liga ilipigwa kwenye Uwanja maarufu wa Camp Nou.

Katika mechi hiyo ambayo mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi alifunga mabao mawili na mengine yakifungwa na David Villa na Alexis Sanchez.


Messi alifunga moja ya mabao bora kwa mkwaju wa adhabu na kufanya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo kuinuka na kushangilia kwa nguvu wakiamini amerejea kazini.

Dimpoz alionekana katika siti za kawaida za mashabiki, si zile ambazo wanakaa watu matajiri.

Alikuwa amevaa jaketi liliondikwa Catalunya ikionyesha naye ni kati ya mashabiki we timu hiyo ya Catalunya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic