May 6, 2013



 Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ametoa kauli iliyowashangaza wengi baada ya kusema hajawahi kuzungumza na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola tokea alipoondoka Barcelona.

Katika mahojiano na 'El Gráfico', Leo Messi alisema hajawasiliana na kocha huyo hata mara moja tokea aachane na Barcelona.

Messi alisema hayo wakati alipoulizwa kama anaona Guardiona anaweza kuifundisha timu ya taifa ya Argentina.


“Sidhani kama atapata nafasi hiyo, sisemi kuwa hawezi kutokana na uwezo. Lakini kwa utamaduni wa Argentina hawawezi kukubali kumpa mgeni timu ya taifa,” alisema.

Kauli yake kwamba hajawahi kuzungumza na Guardiola imewashangaza wengi kwa kuwa ilionekana kocha huyo alikuwa rafiki yake wa karibu wakati wakiwa pamoja Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic