Bondia Francis Cheka amesema hakuna bondia nchini
anayeweza kufanya mazoezi makali kama ambayo amekuwa akiyafanya.
Cheka ambaye siku chache zilizopita alitoa kipigo
kikali kwa Thomas Mashali na kumchapa kwa knockout (KO) katika raundi ya 10.
Akizungumza na Salehjembe, Cheka alisema amekuwa
akifanya mazoezi makali sana chini ya kocha wake Abdallah Saleh maarufu kama
Komando.
“Sidhani kama kuna bondia anaweza kufanya mazoezi
kama mimi, ni makali sana na kocha wangu hataki mzaha hata kidogo.
“Nimekuwa nikipanda milima na hauwezi kuamini,
kocha wangu anachofanya si kwamba yeye anakaa ananisubiri. Badala yake
tunakimbia pamoja.
“Unaweza kudhani anakuwa nyuma, pamoja na kuwa na
umri mkubwa yeye ndiye anakuwa mbele na ninalazimika kumfuata.
“Mazoezi yangu ni makali sana, unatakiwa kuwa
mvumilivu kweli ili kuyafanya na kumaliza hadi mwisho,” anaelezea Cheka.
Kuhusiana na kuendelea kupambana, Cheka alisema
anataka kupumzika kwa muda kabla ya kuendelea kucheza tena.
“Si kwamba nimejiondoa katika ngumi, napumzika tu
kama inavyotakiwa kwa bondia. Unajipa muda kidogo baada ya pambano.”
0 COMMENTS:
Post a Comment