May 5, 2013




Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ametua nchini Uingereza jana jioni tayari kukutana na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short.

Rage anaungana na Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi kufanya mkutano na Short na utafanyika leo na keshokutwa.



Rage aliondoka nchini kimyakimya na kutua nchini humo, taarifa zinaeleza kuwa amefikia katika hoteli ya Ibisi jijini London.

Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu za Simba, kuwa Rage tayari yuko jijini London kwa ajili ya mkutano huo.

“Mkutano utafanyika mjini Newcastle na mwenyekiti tayari yuko Uingereza,” kilieleza chanzo hicho.

“Unajua mwenyekiti aliona ende kwanza bila ya kuitangaza halafu baadaye itajulikana ndiyo maana na sisi tukawa kimya.”

Mmoja wa wadau wa Salehjembe, alisema alimuona Rage katika mitaa ya jiji la London ukiwa ni uthibitisho ameshatua nchini humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic