M To The P akiwa na Ngwea wakiwa jijini Johannesburg siku chache zilizopita |
Pigo tena kwa muziki wa Bongo Fleva baada ya ripoti kusema, M To The P aliyekuwa na Mangwea jijini Johannesburg naye amefariki dunia.
Taarifa kutoka Johannesburg zinaeleza M To The P amefariki dunia baada ya kulazwa katika hospitali ya St Helen Joseph ambayo mwili wa Mangwe umehifadhiwa.
lakini kuna utata kwa kuwa kuna taarifa nyingine zilitufikia punde na kueleza alikwua chumba cha watu mahututi (ICU), hali inayozidi kuleta utata.
Mangwea na M To The P walisafiri pamoja hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya shoo na baadaye waliendelea na maisha yao.
Lakini juzi wakati wanatarajia kurejea nyumbani, Mangwea alikutwa amefariki dunia chumbani na M To The P akiwa taabani na akakimbizwa hospitali.
“Kweli amefariki dunia, ni Yule mwenzake na Mangwea, sasa tuko kwenye pilika ya kuandaa mazishi,” alisema Thomas, mmoja wa Watanzania wanaoshughulikia suala la mazishi.
Tunaendelea kufuatilia kupata uhakika zaidi kuhusiana na M To The P, ili kujua usahihi huo kwa kuwa Watanzania waliokuwa katika hospitali hiyo wanasema wauguzi na madaktari wanawachanganya kuhusiana na ukweli kuhusiana na hilo ingawa kuna wengine wamewaambia msanii huyo pia ameaga dunia.
0 COMMENTS:
Post a Comment