May 28, 2013

Msuva na Domayo (kulia)


Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anajivunia mafanikio waliyoyapata wachezaji wa Yanga, Frank Domayo na Simon Msuva.

Julio amesema Msuva na Domayo wamekuwa makinda waliofanya vizuri kwa msimu mzima na wastahili pongezi lakini yeye ataendelea kujivunia kama mmoja wa makocha waliowapa nafasi alipokuwa nao katika timu za taifa za vijana.
Julio

“Mimi ni kocha wa timu za vijana za taifa, nilikuwa kati ya makocha waliowapa nafasi Msuva na Domayo. Nathubutu kusema najivunia walipofikia.


“Kama nisingetoa nafasi au kocha Kim (Poulsen) asingewaamini, basi leo wasingekuwa hapo. Bado wanatakiwa kufanya vizuri zaidi ya hapo.

“Kikubwa ni kujituma lakini ni makocha pia kujifunza kutokana na vijana hao, hata ukiangalia Simba tumekuwa na vijana waliofanya vizuri sana kwa kuwa tuliwaamini.

“Haina maana wakongwe hawapaswi kuaminiwa lakini vijana pia ni nguzo ya maendeleo katika soka, hivyo kuwaamini ni jambo zuri lakini nao hawapaswi kujisahau mapema. Badala yake wajitume zaidi,” alisema Julio.

Pamoja na hivyo, Julio alisisitiza suala la makocha kupewa nafasi ya kufundisha timu tofauti badala ya kuangalia Uyanga na Usimba ambao alisema unadumaza fani hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic