Simba imemaliza
hofu kubwa kwa mashabiki wao baada ya kufikisha fedha zaidi ya Sh milioni 20
zilizokuwa zinatakiwa kumkabidhi Amri Kiemba ili asaini mkataba mpya.
Kiemba
ambaye amekuwa kiungo bora kwa Simba kwa msimu uliopita alikuwa anawaniwa na
Simba, hali iliyozua hofu kubwa miongoni mwa mashabiki wa Msimbazi.
Wiki
iliyopita, taarifa za Kiemba amesaini Yanga zilizagaa mitaani na kuzua tafrani
kubwa na baadhi walikuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili kutaka kujua
kama kweli kiungo huyo ametua Jangwani.
Lakini
habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, tayari fedha alizotakiwa
kulipwa zimewekwa kwenye akaunti yake na kinachosubiriwa ni kusaini tu.
“Kila kitu
safi, tayari fedha yake iko kwenye akaunti. Kinachosubiriwa hapo ni taratibu za
kibenki tu ili fedha iwe imeingia. Baada ya hapo kuna ndugu yake yuko hapa Dar
es Salaam, atawasiliana na Kiemba na kumuambia kwamba kila kitu safi,”
kilieleza chanzo.
Lakini
awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope alilieleza
gazeti hili kwamba walikuwa wamekubaliana na Kiemba kila kitu.
“Limebaki
suala la kumkabidhi fedha yake tu, lakini tumeelewana naye kila kitu.
Ametuhakikishia hataki kuhangaika nasi tumemkakikishia kumlipa fedha hizo,
hakuna shaka tutamalizana vizuri kwa kuwa tunamuamini,” alisema Hans Pope.
0 COMMENTS:
Post a Comment