May 23, 2013



Rais Kikwete na kikosi cha Taifa Stars..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amewaambia wachezaji wa Taifa Stars kuwa wana uwezo wa kuishinda Morocco katika mechi yao ya Juni 8.

Pamoja na hivyo, Kikwete amesisitiza lazima Ivory Coast watakapokuja nyumbani Dar es Salaam, basi nao wakione cha moto kwa kupata kipigo.


Kikwete aliyasema hayo leo mchana baada ya kuwaalika Stars katika chakula cha mchana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete, ameyasema hayo leo mchana wakati alipokutana na kikosi cha stars, alichokutana nacho kufuatia timu hiyo kualikwa kwa chakula cha mchana, hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar.


Pamoja na kuwapa moyo Stars, Kikwete alimpongeza Kocha Kim Poulsen kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chote ambacho amekuwa kocha.
 
Rais Kikwete akizungumza...

Nahodha Kaseja akizungumza...

.Rais Kikwete na Yondani

...na Barnabas.

...na Kocha Kim Polsen.

..na Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah.

...Barthez.

....Kiemba

Alieleza wazi kuwa kocha huyo amekuwa akiifanya kazi yake vizuri na imeanza kurudisha imani kwa mashabiki walioonyesha kuanza kukata tamaa.

Pia alipongeza suala la kuanzishwa kwa Young Taifa Stars ambayo anaamini itasaidia kujenga Taifa Stars imara zaidi.

Chakula hicho cha mchana kiliwajumuisha viongozi mbalimbali wa Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Watanzania wanataka kuona timu yao inafanya vizuri, hata mkicheza na timu kubwa kama Hispania au Brazil, wao wanataka Stars ishinde na hilo linawezekana. Nataka kuona hata wakija Ivory Coast hapa mnawanyoa hakuna kumuachia mtu, mkiendelea kushinda,  haya mnayoyapata sasa yataongezeka zaidi,” alisema Kikwete.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic