May 23, 2013



 
Pamoja na kuonekana wanaficha mambo kupita kiasi, lakini taarifa za uhakika zinaeleza Real Madrid watamtambulishi kocha wao mpya, Carlo Ancelotti, Jumatatu Juni 3.

Taarifa kutoka ndani ya Madrid zinaeleza kazi hiyo itafanywa na Rais wa kalbu hiyo, Florentino Perez.



Ancelotti ambaye yuko PSG ndiye atakuwa mrithi wa Jose Mourinho ambaye anarejea kujiunga na Chelsea ya England.
 


Perez anaonekana kama atakuwa mgombea pekee wa kiti hicho na ndiyo atamtambulisha Ancelotti ambaye wameishamalizana naye kwa asilimia 95 hadi sasa.

Hata hivyo Madrid wameendelea kutotaka suala hilo lijulikane lakini taarifa zinasema wameishamalizana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic