May 6, 2013



 
Hata kama iwe vipi, kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi ya nchini Argentina haiwezi kuepuka kwamba imempiga madongo Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho.

Pepsi wamefanya kampeni kubwa kama uzinduzi tena wa kinywaji hicho na kumualika kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola kama mgeni wa heshima.

Wakati wa uzinduzi huo, mapango ya Pepsi yalikuwa na maneno yasemayo "Mou no, Pep sí".

Tafsiri ya maneno hayo ni Mourinho hapana, Pep ndiyo.
Ingawa wataalamu wa matangazo wa Pepsi nchini Argentina wamekuwa wakikanusha kutokana na ufundi wao mkubwa walioutumia kuchezea maneno hayo.


Mmoja wa maofisa alisema maana yake ilikuwa ni kama kumkaribisha Guardiola na kuonyesha namna gani Barcelona ilicheza soka safi la kuvutia wakati wa uongozi wake lakini Mourinho ameshindwa kufanya jambo hilo.

Mourinho alikuwa mpinzani mkubwa wa Guardiola kabla ya kocha huyo kuamua kuachia ngazi Barcelona. 

Kabla alionekana Mourinho hana chake, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, Mreno huyo taratibu alianza kupindua kabati kama ‘mende’ jasiri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic