Na Saleh
Ally
KOCHA Mkuu
mpya wa Simba, Abdallah Kibadeni ameanza kazi rasmi baada ya kusaini mkataba wa
miaka miwili na klabu hiyo.
Siku ya
kwanza akiwa kazini na Simba imehusisha kuwafanyia majaribio wachezaji
wanaowania kusajiliwa Simba na raia wanne wa DR Congo wamejitokeza kuwania
nafasi hiyo.
Kibadeni
aliyekuwa kocha wa kagera Sugar msimu uliopita, jana aliliongoza benchi lake la
ufundi akiwa na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ pamoja na makocha wa
timu za vijana na watoto wa Simba, Selemani Matola na Amri Said ‘Stam’ kufanya
kazi hiyo.
Katika
shughuli hiyo iliyokuwa ikifanyika asubuhi kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar
es Salama, Wakongo watano walikuwa ni Patric Milambo kutoka Nguena ya DRC,
Fabrice Baloko (Villa-DRC), Joe Fils, Fabian Tshiyaz (Vita Club,
Lubumbashi-DRC).
Pia
kulikuwa na Adeyun Saleh kutoka Mlandege ya Zanzibar na wote walishiriki katika
kundi la vijana zaidi ya 50 waliojitokeza kuwania nafasi ya kuichezea Simba.
“Ndiyo
tunaanza kazi hii ya vijana, lakini mimi tayari nimesaini mkataba wa miaka
miwili na Simba,” alisema Kibadeni.
Salehjembe:
Makocha hupenda kuhama na wasaidizi wao, unawaleta wa Kagera?
Kibadeni:
Hapana, mimi, Julio, Matola na wengine tunatosha sana. Watuamini tu.
Salehjembe:
Unahisi hawawaamini?
Kibadeni:
Inawezekana, unajua nimefanikiwa Kagera kwa kuwa nilikuwa napanga timu
mwenyewe. Sipendi kupangiwa timu, mfano nisikie sijui mwenyekiti anataka
mchezaji fulani acheze, sitakubali.
Salehjembe:
Unafikiri unahitaji muda gani kubadili Simba?
Kibadeni:
Muda ni kawaida, lakini lazima kuwe na uvumilivu na watuamini tutengeneze timu,
hatuwezi kufeli.
Salehjembe:
Usajili unaofanyika unakuridhisha?
Kibadeni:
Sasa siwezi kusema, wachezaji nitawaona uwanjani na kwa kuwa tuna muda, basi
nitajua cha kufanya. Vizuri tutakuwa na muda wa kujirekebisha na michuano ya
Kagame, Sudan pia itatusaidia kuijua timu yetu vizuri.
Salehjembe:
Kila la kheri katika kazi yako mpya.
Kibadeni:
Nashukuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment