Uongozi wa Simba umesema tayari umeamua kuachana na kipa wake Juma Kaseja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope ameiambia Salehjembe kwamba tayari wameamua kuachana na kipa huyo maarufu kuliko wote nchini katika kipindi hiki.
“Tunapenda kutangaza rasmi kwamba tumeachana na Kaseja na hatutamuongezea tena mkataba.
“Hivyo kama ataona anataka kusajili timu yoyote, basi awe huru kufanya hivyo, sisi hatutamsajili,” alisema Hans Pope.
Hans Pope amesema wamefikia uamuzi wa kumuacha Kaseja baada ya kukaa na kujadili, hivyo kuona hakuna haja ya kujadili kesho katika kikao cha kamati ya utendaji.
“Wajumbe wa kikao kesho wataelezwa kwamba hilo limeishapitishwa kwa kuwa hata benchi la ufundi nalo lilitoa maoni yake,” alisema Hans Pope.
Kwa kumuacha Kaseja, Simba inabaki na makipa wawili, Abel Dhaira raia wa Uganda pamoja na Ntalla ambaye imemsajili msimu huu kutokea Kagera Sugar.
"It is not fair"...hata kama ana mapungufu yake lakini Kaseja ameifanyia mengi sana Simba tena mazuri. Haiwezekani leo hii Ryan Giggs aachwe na Manchester United kihunihuni kama viongozi wa Simba walivyofanya kwa Kaseja. Hili ndio soka la Bongo..miaka 10000 tutabaki hivihivi na upumbavu wetu.
ReplyDeleteInasemekana kaseja aliringa, na kwa maoni yangu aliringa wakati mbaya kwa sababu simba tayari ina kipa mdogo waliyemsajili kwa hela nyingi na wanamlipa hela nyingi, na ni kipa wa taifa pia (dhaira). Pengine kaseja mwenyewe naye ni wa kujilaumu. Mpira biashara siku hizi
ReplyDelete