Bao
lililofungwa kwa kichwa na Paulinho katika dakika ya 86, limeipeleka Brazil
hadi fainali ya michuano ya Kombe la Mabara.
Brazil
imefanikiwa kutinga fainali baada ya kuifunga Uruguay kwa jumla ya mabao 2-1.
Brazil
walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 41 kupitia Fred baada ya kazi
nzuri ya Neymar lakini Uruguay wakasawazisha katika dakika ya 48 baada ya
mabeki wake kufanya makosa na mara moja Cavani akafunga.
Mechi
hiyo ilikuwa ni ya vuta nikuvute na Uruguay ndiyo walianza kupata nafasi ya
kufunga baada ya mwamuzi kuwapa mkwaju wa penalty baada ya David Luiz kufanya
madhambi ndani ya 18.
Lakini
mkwaju wa mkongwe Diego Forlan ukaolewa na kila Julio na kufanya ugumu wa mechi
uendelee hadi mwisho Brazil walipofanikiwa kuibuka na ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment