Kikosi cha Ivory Coast kitaondoka
mara moja mara baada ya mechi ya Taifa Stars kesho kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
Bado haijajulikana kama watarudi
tena hotelini Bahari Beach, lakini taarifa zinaeleza baada ya mechi huenda
wakaunganisha moja kwa moja hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
na kuondoka zao.
“Kweli baada ya mechi hatutalala
Tanzania,” alisema mmoja wa maofisa wa timu hiyo kambini kwao Bahari Beach.
“Huo ndiyo umekuwa uamuzi na
tunalazimika kufanya hivyo kwa kuwa tumekuja na ndege ya kukodi ambayo
tutandoka nayo.
“Tunaona ni vizuri kufanya hivyo kwa
maana ya muda, lakini bado wachezaji wengi wanacheza nje ya Ivory Coast na
wangependa kuwahi kurudi katika mapumziko na baadaye kujiunga na timu zao kwa
maandalizi ya msimu mpya,” alisema.
Mechi ya kesho inasubiriwa kwa hamu
kubwa na Stars inatakiwa kushinda ili kujiweka kwenye njia ya kuendelea kuwania
kucheza Kombe la Dunia.








0 COMMENTS:
Post a Comment