Juhusi
za Kocha Mpya wa Man United, David Moyes zimegonga mwamba baada ya Everton
kusema haimuuzi beki wake wa kushoto, Leighton Baines.
Everton
imeiambia Man United iliyotoa ofa ya pauni milioni 12 kwamba haina mpango wa
kumuuza beki huyo.
Moyes
aliyejiunga na United akitokea Everton ndiye alikuwa akimtaka beki huyo lakini
klabu hiyo imesema hauzwi.
Imeelezwa
Kocha Mpya wa Everton, Roberto Martinez naye amesisitiza beki huyo asiondoke
ili kujenga kikosi imara zaidi.
Uongozi
wa Everton umeishatangaza kwamba unataka kubaki na Baines ambaye anaonekana
kumpa shida Ashley Cole katika namba tatu katika kikosi cha timu ya taifa ya
England.
0 COMMENTS:
Post a Comment