Hispania
imefanikiwa kusonga hadi fainali ya Kombe la Mabara baada ya kuifunga Italia
kwa mikwaju 7-6 ya penalti.
Mechi
hiyo kali ilimalizika kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika
120 bila bao.
Sasa
Hispania inakutana na wenyeji Brazil katika mechi ya fainali itakayopigwa
kwenye Uwanja wa Maraccana Jumapili.
Katika
penalti tano za mwanzo timu zote zilifunga baada ya kila upande ulipata na
zilipofika za sita, kila upande ukafunga pia.
Lakini
ilipofikia penalty ya saba, Italia wakakosa na Jesus Navas akafunga ya mwisho
na kuipa ushindi Hispania.
Awali,
mechi hiyo hiyo ilikuwa kali na ya kusisimua na si kama ambavyo ilivyoonekana
awali kwamba ingekuwa mchekea kwa mabingwa wa Dunia, Hispania.
Italia
ilicheza bila ya mshambuliaji wake nyota, Mario Balotelli na ilionyesha soka la
uhakika na kuwapa wakati mgumu Hispania.
Mechi
hiyo ilimalizika sare ya bila bao katika dakika 90 na zilipoongezwa dakika 30,
bado matokeo yakabaki kuwa hayo.
Timu
hizo zikaingia katika mikwaju ya penalti na kabla ya kuanza kupiga, kipa Buffon
wa Italia alionekana kulalama ingawa haikujulikana alikuwa akilalama kitu gani.
Mara ya mwisho Hispania kupoteza mechi kwa mikwaju ya penalti ilikuwa mwaka 2002 katika Kombe la Dunia dhidi ya Korea.
Msanii
maarufu wa pop, Shakira ambaye alikuwa jukwaani, alikuwa kivutio kila
alipoonyesha.
Shakira
alikuwa uwanjani hapo kumuunga mkono mpenzi wake Gerard Pique ambaye ni beki wa
kati wa Hispania na Barcelona.
0 COMMENTS:
Post a Comment