Mabingwa
wa soka Tanzania, Yanga wameamua kuboresha zaidi safu yao ya ulinzi baada ya
kumsajili kipa Deo Munishi maarufu kama Dida.
Mmoja
wa ‘majembe’ ya Yanga katika suala la usajili, Abdallah Bin Kleb amethibitisha
kumsajili Dida.
“Kweli
tumemsajili Dida, tumempa mkataba wa miaka miwili na lengo letu ni kuimarisha
safu ya ulinzi.
“Hivyo
Dida atashirikiana na Barthez kuimarisha ulinzi katika lango la Yanga,” alisema
Bin Kleb.
Dida
alikuwa kipa wa Azam FC, lakini timu yake hiyo haikumpa mkataba baada ya
kuingia katikam mgogoro kutokana na shutuma za kupanga matokeo.
Azam
FC ililifikisha suala hilo kwa Taasisi ya Kupamabana na Kuzuia Rushwa
(Takukuru) na baada ya muda majibu yalitoka Dida na wenzake Erasto Nyoni, Agrey
Morris na Said Morad hawakuwa na hatia.
Kabla
ya kutua Azam FC, Dida alikuwa kipa namba moja wa Mtibwa Sugar aliyojiunga nayo
akitokea Simba alikokuwa kipa namba tatu chini ya Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Maana
yake Dida amekutana na Barthez kwa mara nyingine tena, safari hii wakiwa makipa
wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment