Italia imefanikiwa
kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mabara baada ya kuichapa
Uruguay kwa mikwaju 3-2 ya penalty.
Mechi hiyo
imemalizika kwa dakika 120, timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Italia ilikuwa
ya kwanza kupata bao kupitia kwa Astori katika dakika ya 24, Cavani
akaisawazisia Uruguay katika dakika ya 58.
Ilipowadia dakika
ya 73, Italia wakatangulia kwa mara ya pili kwa bao lililofungwa kwa mkwaju wa
faulo na Diamant lakini Cavani tena akajibu katika dakika ya 78 kwa mpira wa
faulo pia.
Katika mikwaju
ya penalti, kipa mkongwe na nahodha wa Italia, Buffon aliibuka shujaa baada ya
kupangua na kudaka penalti tatu ikiwemo ya mkongwe Diego Forlan.
0 COMMENTS:
Post a Comment