Samatta (kushoto) akiwa na Ulimwengu (kulia) na Sure Boy katika kikosi cha Taifa Stars |
Washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wako nchini Ghana kujiandaa na mechi za robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Samatta na Ulimwengu wako mjini Accra na kikosi cha TP Mazembe ambako watakuwa wakifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Setif na Watanzania hao wanaonekana kuwa tegemeo la ushambuliaji kwa kushirikiana na Tresor Mputu na Mzambia, Given Singuluma.
Katika kikosi hicho kilichoondoka mjini Lubumbashi, juzi na kutua Kinshasa kwa muda kabla ya kumaliza safari yake jijini Accra, kocha wa Mazembe aliamua kumuacha kiungo wake Patrick Ochan na mwenzake Mike Mutyaba.
TP Mazembe itaanza kibarua cha robo fainali kwa kucheza na Setif, hiyo itakuwa Julai 19 na inaonyesha wazi mechi ya kwanza ndiyo itatoa majibu kwao.
Mazembe wakiwa mjini Accra watakuwa wakicheza mechi Julai 19 na imekuwa ni kawaida kwa timu hiyo kuweka kambi mjini humo ili kujiimarisha kabla ya mechi zake muhimu.
Wababe hao wa DR Congo wamerejea hadi katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuporomoka kutoka Ligi ya Mabingwa kutokana na kutolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza wakilala kwa mabao 3-1 jijini Johannesburg kabla ya kushinda 1-0 mjini Lubumbashi wakiwa wamekosa penalti katika mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment