Inaonekana
wazi kuwa Ivory Coast hawaichukulii kilahisi mechi dhidi ya Taifa Stars, kwani
hawajataka hata kidogo kuonyesha wanafanya nini.
Jana
wamesusia, hawakutokea katika mazoezi ya timu yao ambayo yalipangwa kufanyika
kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar,
Lakini leo
viongozi wao hawakutokea katika mkutano wa waandishi wa habari bila ya taarifa
yoyote.
Mambo hayo
mawili yanaonyesha kuwa Ivory Coast haitakuwa na mzaha na mechi hiyo ya kesho
dhidiya Taifa Stars.
Badala yake
jana, Salehjembe ilishuhudia wakifanya mazoezi mepesi ya kupiga danadana karibu
na ufukwe wa hoteli ya Bahari Beach waliyofikia.
Lakini kwenye
mkutano, Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen na nahodha Juma Kaseja ndiyo walifika
pale na hakuna aliyejitokeza kutoka kwa wageni hao.
Katika mechi
ya mjini Abidjan, Stars ililala kwa
mabao 2-1 tena kwa taabu sana, hivyo kikosi hicho wanajua kwamba kazi si lahisi
kwa kuwa Stars wako sawa.
Ila uhakika,
Ivory Coast watafanya mazoezi leo na tayari watu wao wawili walikwenda kuukagua
uwanja.
Jana walifanya
hivyo kwenye Uwanja wa Gymkhana, halafu wakayeyuka tu bila ya kufanya kitu
chochote na timu haikutokea.
Stars inahitaji
ushindi kuzidi kuweka matumaini, kama itapoteza mechi ya kesho, maana yake
itakuwa imejitoa katika mbio za kuwania kwenda Brazil.
0 COMMENTS:
Post a Comment