Mbunge wa
Kawe (Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi dhidi
ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
Pambano la
wakali hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini
kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.
Mdee
amekuwa akiendelea na mazoezi yake chini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye anaamini bondia wake siku hiyo atatoa funzo kwa Wolper.
Katika tamasha
hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao
lililosisimua.
Lakini Mdee
ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee
anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini
Dar es Salaam.









0 COMMENTS:
Post a Comment