Kocha Mkuu wa
Ivory Coast, Sabri Lamouchi amesema hawaichukulii kwa utani mechi ya leo kwa
kuwa ni kama fainali.
Lakini Kocha
wa Stars, Kim Poulsen amesema wanachotaka ni ushindi kwa kuwa wakishindwa leo,
basi mechi dhidi ya Gambia itakuwa ni sawa na ya kujifurahisha tu.
“Heshima
yetu kwa Tanzania ni kubwa sana, lakini tunajua umuhimu wa mechi hii. Kazi yetu
kama wanaume ni kupambana uwanjani na ndicho tutakachofanya,” alisema Lamouchi
ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Tunisia aliyekuwa kiungo nyota
katika timu za Ales, Auxerre, Monaco za Ufaransa, Parma na Inter Milan za
Italia. Pia timu ya taifa ya Ufaransa.
Lamouchi alikuwa akiwindwa na waandishi kwa kuwa hakutokea katika mkutano wa waandishi, hivyokufanya watu wasipate neno lake kuhusiana na mechi hiyo.
Katika mahojiano
hayo, mengine ambayo yatatoka katika gazeti la CHAMPIONI la keshi Jumatatu,
Lamouchi pia amemzungumzia mshambuliaji Didier Drogba na beki Kolo Toure.
Kwa upande wa
Poulsen alisema mechi ni ngumu kwa kuwa wanacheza na wajuzi lakini kikosi chake
kitacheza kama timu.
“Tunajua
umuhimu wa ushindi wa leo, kila mmoja anataka kushinda na tunajua hauwezi
kupatikana bila ya sisi kushirikiana uwanjani,” alisema Mdenishi huyo.
TAYARI
IVORY COAST WAKO NJIANI KUELEKEA TAIFA NA BAADA YA MECHI WATAONDOKA KWENDA KWAO
IVORY COAST.







0 COMMENTS:
Post a Comment