Katika
mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast, pamoja na kupoteza kwa kufungwa
kwa mabao 4-2, uwanjani kulikuwa na ushirikiano wa hali ya juu kabisa.
Mashabiki
wengi waliojitokeza waliendelea kuua utamaduni mbovu wa miaka michache
iliyopita ya kila upande hasa Yanga na Simba kushangilia wachezaji wao.
Wakati
Fulani ilifikia, Yanga wanashangilia wachezaji wao na kuwazomea wa Simba bila
ya kujali wanachezea timu ya taifa, halikadhalika Simba walifanya hivyo pia.
Hakikuwa
kitu kizuri, kilileta mgawanyiko, msawijiko na mshangao kwa wengi wenye utaifa.
Lakini
sasa ni raha na mambo yamebadilika, inawezekana kabisa mambo yakabadilika na
Yanga na Simba siku moja wakaungana na kuizomea timu ya ugenini.
Angalia
picha hii inavyoonyesha, mashabiki wa Simba na Yanga wameunganisha bendera zao
na kuishangilia Taifa Stars.
Hili
ni jambo la faraja sana, linaweza kuonekana ni kitu kidogo, lakini maana yake
ni kubwa sana kwa maana ya utaifa.
Labda
tuendelee kusubiri, siku moja pale mashabiki wa timu hizo mbili kubwa hapa
Tanzania watakapoungana na kuizomea timu ya nje na siku nyingine upande
mwingine ukausaidie mwingine na mwisho uwe utamaduni.
Katika
pitapita zangu, nimeshuhudia suala hilo katika nchi tatu, kwanza Misri, pili
Tunisia na tatu Rwanda. Maana yake hata Tanzania inawezekana.
0 COMMENTS:
Post a Comment