Mara
kadhaa kumekuwa na malalamiko kuhusiana na mambo yalivyo katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Ninamaanisha
waharibifu wa mali za uwanja huo hasa wale ambao wamekuwa wakikosa ustaarabu na
wanaotaka kuonekana machoni mwa watu.
Wanafanya
hivyo kwa kuwa wanataka kupata umaarufu wa haraka, hata kama mwamuzi atakosea,
wakiamini ‘wanaumwa’, basi mara moja wanaanza kuvunja viti.
Jiulize
hasira zao na viti zinaendana vipi, kwa kifupi ni kutaka kuonekana ni kama wale
watu wa Ulaya kwa kuwa wamewaona kwenye runinga waking’oa vipi, huo ni upuuzi.
Watu
wa hivyo, tumekuwa tukiwapiga vita na lazima wajizuie na hasira hizo, au
wachague kubaki nyumbani ili wauache salama Uwanja wa Taifa ili utumiwe na
wadogo zetu na ikiwezekana baadaye watoto zetu kama ambavyo tulivyoukuta Uwanja
wa Uhuru.
Pamoja
na hao, uchunguzi wa Salehjembe umeonyesha kuna mambo kadhaa yanatakiwa
kufanywa na serikali kuhusiana na uwanja huo.
Ukarabati
wa mara kwa mara, kaka ukiangalia utaona uwanja huo unaanza kupata kasoro
kadhaa zinazoashiria matengenezo.
Inawezekana
serikali haijaona, lakini inaendelea kufurahia vitita vya fedha zinavyoingizwa
na uwanja huo ghali zaidi Afrika Mashariki na Kati.
Mfano
mzuri kama picha zinavyoonyesha, hayo ni mabenchi ya huo uwanja ambayo makocha
na wachezaji wa akiba hukalia.
Yanaonekana
yameanza kuoza na kutu na huenda baada ya muda yakameguka, lakini wahusika wa
uwanja hawajaliona hilo.
Au
inawezekana wameliona lakini wanapuuzia, siku zote kutu hutakiwa kuwahiwa
mapema. Hivyo ni lazima waanze sasa na si kusubiri.
Ukarabati
wa kutu ukifanyika mapema, hata gharama hupungua, ila unavyozidi kuachwa ndiyo
tatizo kubwa zaidi.
Picha
hizi haziongopi, kila kitu kinaonekana na wahusika walifanyie kazi mara moja suala
hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment