Kocha wa
zamani wa Simba, Patrick Liewig alikuwa hajui kama tayari Ngassa ameishajiunga
na Yanga.
Liewig
alisema anataka kuwaona wachezaji wake wa zamani akiwemo Ngassa.
Lakini alipoambiwa
Ngassa ameshajiunga na Yanga, alionekana kushangazwa na hali hiyo.
“Basi mimi
sijui, lakini siwezi kuzuia. Hata kama ameenda lakini vizuri Simba
wangembakiza.
“Ukitaka
kumsajili mchezaji anayemaliza mkataba, vizuri ufanye naye mazungumzo ndani ya
miezi sita.
“Ngassa ni
mtu mzima anaweza kuamua anachotaka, lakini ndiyo hivyo,” alisema.
Ngassa
alijiunga na Yanga rasmi mara tu baada ya mechi dhidi ya Simba, lakini
inaonekana Liewig hakuelewa lolote.
Liewig
yuko nchini kudai fedha zake kutoka kwa uongozi wa Simba ambao umeingia mkataba
na Abdallah Kibadeni kama kocha mkuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment