June 13, 2013

Wakati timu ya Ivory Coast inatarajiwa kuwasili leo usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, tiketi kwa ajili ya mechi kati yake na Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa zinaanza kuuzwa kesho mchana (Juni 14 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vituo vitakavyotumika kwa mauzo hayo ni Shule ya Sekondari 

Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa 
wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, 
Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza  Madukani.

Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda  

ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, 
sh. 7,000
 viti vya rangi ya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, 
sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa 
sh. 30,000.

Pia viti 100 vilivyo katika sehemu ya Wageni Maalumu (VVIP) 

vitauzwa kwa sh. 50,000 kila kimoja. Tiketi hizo zitauzwa katika 
ofisi za TFF, 
na watakaonunua watapewa kadi maalumu zenye majina yao, 
majina ambayo pia watayakuta katika vita watakavyokaa. Kwa 
maana hiyo hakutakuwa pasi maalumu  (free pass) za kuingia VIP.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic