Kocha Patrick Liewig tayari ametua
jijini Dar es Salaam kuendelea na kazi ya kuinoa.
Liewig amesema amekuja kuendelea na
kazi yake kwa kuwa yeye ndiye kocha mkuu wa Simba.
“Mimi ndiyo kocha, nitaanza kazi leo au
kesho. Nimejua wanafanya mazoezi Kinesi. Nitakwenda kuanza kazi,” alisema.
Alisema anashangazwa na kuona viongozi wa
Simba wanaonyesha kumkwepa, lakini hajali.
“Niko hotelini hapa Kariakoo, inaitwa
Supphire. Hivyo nitaendelea kuwa hapa huku nikiwatafuta viongozi,” alisema.
Tayari Simba imeishangia mkataba wa
miaka miwili na Abdallah Kibadeni kuinoa Simba.
Mkataba wake unaonyesha, Simba
wanalazimika kumlipa mshahara wa miezi miwili ambao ni dola 12,000.
Simba ilimuondoa Milovan Cirkovic kwa
mtindo huo, lakini alirejea kutoka kwao Serbia na kudai mshahara wake hadi
alivyolipwa na Malkia wa Nyuki dola 35,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment