Na Saleh Ally, Freiburg, Ujerumani
Vijana wa Kitanzania
wanaofaya mafunzo ya kisasa kupitia FELS Project wamekuwa wakiendelea kufaya
vizuri,
Mafunzo ambayo
wanafanya yamekuwa ni ya aina mbalimbali yakiwemo yale ambayo ni adimu
kufanyika nyumbani.
Chini ya Kocha
Alex aliyeshirikiana na Jurgen waliwafundisha namna ya kucheza kwa hisia hali
inayomfanya mchezaji kuwa na kasi kwa kuwa mchezo wa soka unaendana na hisia.
Wachezaji hao
sita makinda kutoka Tanzania walikuwa wanafunikwa vitambaa usoni na kuruka
vifaa maalum ili kuonyesha uwezo wa hisia zao.
Kwamba mchezo wa
soka pamoja na kuona lakini zaidi unatakiwa kuhisi haraka ili kuweza kuchukua
uamuzi wa haraka unaokuwa na faida kwa timu yako na madhara kwa wapinzani.
0 COMMENTS:
Post a Comment