Timu ya Toto African ya Mwanza imeendelea kuwa katika
wakati mgumu kutokana na kukimbiwa na wbaadhi ya wachezaji ikiwa ni muda mfupi
baada ya kushuka daraja kutoka Ligi kuu Bara na kutakiwa kucheza Ligi Daraja la
Kwanza.
Toto ambayo maskani yake ni jijini Mwanza, imeondokewa
na wachezaji wake sita ambao wametua kwenye timu nyingine.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha wa Athumani
Bilal ‘Bilo’ alisema wachezaji hao walikuwa tegemeo kwenye kikosi chake
wameondoka na anafikiria kingine cha kufanya juu ya mbadala wao.
Amewataja wachezaji walioondoka na timu walizoelekea
Peter Mutabuzi (Kagera), Selemani Jingo (Kagera), Erick Muloko, James Madafu
(Prison), Musa Said (Kagera) na Simba Boaz aliyejiunga Rhino Rangers.
“Nikiwa kocha kuna kazi ya kuziba mapengo hayo kwa
kufanya usajili wa wachezaji wengine ili turejee Ligi Kuu Tanzania Bara,”
alisema Bilal ambaye aliongeza kuwa ameshaanza mazoezi na kikosi hicho kwenye
Uwanja wa Nyamagana.
SOURCE: CHAMPIONI.
0 COMMENTS:
Post a Comment