Kikosi cha Wabunge wa Yanga kitakachocheza mechi
katika tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam kimeongeza nguvu.
Kikosi hicho cha Wabunge wa Yanga kitakachovaana na
wale wa Simba, kimeongeza nguvu kwa kuwachukua Ally Mustapha ‘Barthez’, Athumani
Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa.
Maana yake kikosi hicho kitakuwa na nguvu zaidi ya
kuhakikisha kinawalaza Simba ambao mwaka jana walishinda kwa mikwaju ya penalty.
Imeelezwa hata Simba pia wanaruhusiwa kuongeza
wachezaji kwa idadi kama waliyoongeza Yanga ili kujiimarisha zaidi.
Kikubwa ni timu hizo kuchukua wachezaji kutoka Simba
na Yanga kwa lengo la kujiimarisha zaidi na kujiweka safi kabla ya mechi hiyo.
Tayari mechi hiyo ni gumzo kubwa na kila upande
umepania kushinda ili kuweka heshima lakini Yanga inataka kushinda lakini pia
kulipa kisasi.
Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka, linajumuisha
michezo mbalimbali pamoja na burudani za kila aina zitakazoanzaa siku hiyo ya
sabasaba, asubuhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment